From 30/ August 2026  - 14 September 2026 - Arusha Tanzania?

8
:
88
:
88
:
88

 

TAMASHA LA KIMATAIFA LA HISTORIA LA JULIUS KAMABARAGE NYERERE

 

 

Safari ya Afrika kuelekea uhuru ni simulizi ya ujasiri, kujitolea, na maonoyasiyoyumba. Kuanzia kwenye mapambano ya wazi hadi meza za diplomasia, viongoziwa ukombozi wa Afrika walisimama kidete dhidi ya ukoloni, wakawasha moto wauhuru unaoendelea kuwaka hadi leo.

Kuwaenzi Viongozi wa Afrika Walioongoza Harakati za Ukombozi

Safari ya Afrika kuelekea uhuru ni simulizi ya ujasiri, kujitolea, na maonoyasiyoyumba. Kuanzia kwenye mapambano ya wazi hadi meza za diplomasia, viongoziwa ukombozi wa Afrika walisimama kidete dhidi ya ukoloni, wakawasha moto wauhuru unaoendelea kuwaka hadi leo.

Viongozi hawa—wanaume na wanawake wakiwa na msimamo thabiti hawakupiganiamaslahi binafsi. Walitamani heshima kwa watu wao, mshikamano wa mataifa yao, namustakabali unaoongozwa na Waafrika wenyewe. Kutoka hekima ya Mwalimu JuliusKambarage Nyerere katika kuunganisha Tanzania, hadi wito wa Kwame Nkrumah waUmoja wa Afrika, kutoka kilio cha haki cha Patrice Lumumba hadi moyo ya msamahana maridhiano wa Nelson Mandela -urithi wao unaishi.

Katika Tamasha la Kimataifa la Historia la JUKANYE 2026,tunatoa heshima kwa mashujaa hawa. Kupitia simulizi, maonyesho, muziki, Semina nasherehe za kitamaduni, tunakumbuka na kusherehekea kujitoa kwao, tukiwakumbushakizazi cha sasa na kuhamasisha kizazi kijacho moyo wa uzalendo.

 

Majina yao yavume.

Hadithi zao zitutie moyo

.

Maono yao yaendelezwe.

Features

 

TUZO YA MAMA AFRIKA KWA UKOMBOZI NA URITHI

Orodha ya Wanawake Mashujaa wa Ukombozi wa Afrika

Katika kuenzi mchango mkubwa wa wanawake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, tunatarajia kutoa Tuzo za Heshima maalum wakati wa Tamasha la JUKANYE INTERNATIONAL HISTORY FESTIVAL – 2026.

Tuzo hii itatambua na kuthamini juhudi, ujasiri, na urithi wa wanawake waliopigania uhuru na haki za watu wa Afrika katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kijamii na kitamaduni.

Tuzo Maalum: TUZO YA MAMA AFRIKA KWA UKOMBOZI NA URITHI
(Mama Afrika Award for Liberation and Legacy)

 

Tuzo hii ni ishara ya heshima kwa wanawake waliobeba jukumu la kihistoria katika kujenga Afrika huru, yenye utu, mshikamano, na maendeleo endelevu.

Malengo na Matukio

 

 

Malengo ya JUKANYE International History Festival

  •  
  • Kuhifadhi Historia ya Ukombozi wa Afrika
  • Kukuza uelewa wa vizazi vijavyo kuhusu historia ya ukombozi wa bara letu.
  • Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi
  • Kuhamasisha vijana kushiriki katika sekta za uchumi na teknolojia.
  • Kuimarisha Amani na Haki
  • Kujenga jamii yenye mshikamano, haki na mazingira bora ya maendeleo.
  • Kukuza Kiswahili na Utamaduni wa Afrika
  • Kukitangaza Kiswahili kama lugha ya umoja na urithi wa bara letu.
  • Kujenga Ushirikiano wa Kisekta
  • Kuunganisha sekta za utalii, sanaa, elimu, makumbusho na nishati.
  • Kuhamasisha Uzalendo na Bidii
  • Kuwalea vijana wenye moyo wa kujituma na mapenzi kwa nchi zao.
  • Kulinda Mali Asili na Mazingira
  • Kukuza matumizi ya nishati salama na kuhimiza uhifadhi wa mazingira.
  • Kuwezesha Vijana na Ubunifu
  • Kuanzisha mfuko wa kusaidia vijana wabunifu na kuwaunganisha na fursa.
  • Kuimarisha Sekta ya Makumbusho
  • Kuyaboresha makumbusho na maeneo ya kihistoria kwa njia za kidijitali.
  • Kuwa Chanzo cha Mapato na Ajira
  • Kupanua masoko, kuongeza ajira, na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.
  • Kuendeleza Maono ya Mwalimu Nyerere
  • Kutekeleza maono ya umoja, maendeleo, na mshikamano wa Afrika.

 

Matukio na Shughuli Kuu za Tamasha la JUKANYE 2026

 

  • Matukio na Shughuli Kuu za Tamasha la JUKANYE 2026
  • Maonesho ya Makumbusho ya Historia ya Viongozi wa Afrika
  • Yatahusu maisha, fikra na mchango wa viongozi mashuhuri kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Nelson Mandela, Kwame Nkrumah na wengine waliopigania uhuru wa Afrika.
  • Burdani za Muziki wa Asili na Kisasa kutoka Mataifa Mbalimbali
  • Vikundi mbalimbali vya muziki kutoka ndani na nje ya Afrika vitatumbuiza kwa nyimbo za asili na kisasa zenye ujumbe wa umoja, uzalendo na maendeleo.
  • Michezo ya Kuigiza Maudhui ya Historia
  • Tamthilia zenye kuelezea harakati za ukombozi wa Afrika na changamoto zilizokuwepo, zitakazosaidia kuibua uelewa wa kihistoria kwa njia ya sanaa.
  • Maonyesho ya Mavazi ya Kitamaduni na Tamaduni za Nchi Shiriki
  • Kila nchi shiriki itaonesha utajiri wa mavazi na mila zao, kudhihirisha utofauti na mshikamano wa bara la Afrika.
  • Makongamano kwa Vijana na Wadau wa Historia
  • Majadiliano ya kitaalamu yatatoa fursa kwa vijana na wataalamu kuchambua masuala ya maendeleo, ukombozi wa kisiasa na kiuchumi barani Afrika.
  • Kliniki ya Afya kwa Jamii
  • Huduma za afya bure kwa jamii zitapatikana, ikiwa ni sehemu ya kukuza maendeleo ya watu kupitia huduma bora za afya.
  • Ziara za Historia: Butiama, Tabora, Dar es Salaam na Mikoa ya Kusini
  • Ziara maalum kwenye maeneo yenye historia ya harakati za ukombozi kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.
  • Ziara za Kitalii
  • Utembeleaji wa vivutio vya utalii kama Mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar, hifadhi za Taifa, mapori ya akiba, misitu na makumbusho.
  • Kampeni ya Matumizi ya Nishati Salama ya Kupikia
  • Elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutumia nishati salama na rafiki kwa mazingira majumbani na katika biashara.
  • Uzinduzi wa Makala Maalum ya Mwalimu Julius Nyerere
  • Filamu au makala mahsusi kuhusu maisha, falsafa na mchango wa Baba wa Taifa kwa maendeleo ya Afrika.
  • Madarasa ya “Tuseme Kiswahili” kwa Wageni kutoka Mataifa Mbalimbali
  • Fursa kwa wageni kujifunza Kiswahili, ili kuongeza matumizi ya lugha hii kama chombo cha mawasiliano barani Afrika.
  • Utoaji wa Tuzo za Heshima
  • Kuwatambua na kuwapa heshima viongozi wa zamani na wa sasa, wanamuziki, na watu waliotoa mchango mkubwa katika kuhamasisha uzalendo, amani, na maendeleo kupitia kazi zao.

Wito wa Ushiriki na ufadhili

 

 

Tunakaribisha ushirikiano na msaada kutoka kwa sekta zote na wadau mbalimbali ili kufanikisha tamasha hili la kihistoria. Ushiriki wako utachangia kuhifadhi historia ya ukombozi wa Afrika na kuhamasisha kizazi kijacho. Tunakaribisha:

 

  • Ushirikiano imara kati ya serikali na sekta binafsi

  • Msaada na ushirikiano kutoka kwa mashirika ya kimataifa

  • Ufadhili wa kifedha na vifaa kutoka kwa taasisi na watu binafsi

  • Ushiriki wa wadau wa vyombo vya habari na mawasiliano ili kufikisha ujumbe wetu kwa jamii pana

  • Ushiriki wa wanahistoria, wasanii, wanataaluma na vijana wenye shauku ya maendeleo ya Afrika

  • Ushirikiano kutoka kwa jamii za ndani na washiriki kutoka pembe zote za dunia

Timu Yetu:

 Kamati kuu ya tamasha itajumuisha wajumbe kutoka JACI, Catz Company Limited, viongozi wa sekta mbalimbali za serikali, mashirika ya kimataifa, na wataalamu kutoka sekta ya Utamaduni, Nishati, Utalii na Elimu. 

Mialiko na Itifaki

 

  • Kuratibu Mialiko Rasmi:
  • Kuandaa na kutuma mialiko kwa wageni wa heshima wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa, mabalozi, mashujaa wa ukombozi, wasanii, na wadau wakuu wa tamasha.
  • Kuhakikisha Itifaki Inazingatiwa:
  • Kuratibu mapokezi ya wageni maalum kwa kufuata taratibu za heshima na hadhi zao.
  • Kuhakikisha taratibu za kitaifa na kimataifa za itifaki zinafuatwa ipasavyo kwenye hafla rasmi.
  • Kurahisisha Uratibu wa Wageni Maalum:
  • Kupanga ratiba, usafiri, malazi, na ulinzi wa wageni mashuhuri wanaoshiriki tamasha.
  • Kuwapa taarifa muhimu wageni kuhusu programu ya tamasha na mahitaji yao binafsi.
  • Kuhakikisha Uwasilishaji Bora wa Hotuba na Heshima:
  • Kusimamia mpangilio wa hotuba, utoaji wa tuzo, na matukio mengine ya hadhi ya juu.
  • Kuandaa watangazaji au wahudumu wa hafla wenye uelewa wa lugha na mila za itifaki.
  • Kuwezesha Ushirikiano wa Kimataifa:
  • Kufanikisha ujio na ushiriki wa wageni kutoka nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kusaidia utoaji wa viza na taarifa za kiusalama na mahitaji maalum.

CONTACT:

Nishati Endelevu na Uhamasishaji wa Matumizi Salama ya Nishati

  • Kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia majumbani
  • Kutoa elimu kuhusu athari za matumizi ya kuni na mkaa kwa mazingira na afya.
  • Kuelimisha jamii juu ya faida za kutumia majiko banifu, gesi safi (LPG), umeme, na nishati jadidifu kama vile sola.
  • Kushiriki katika maonyesho ya teknolojia za nishati safi
  • Kuonyesha bidhaa na teknolojia zinazochangia matumizi salama ya nishati, zikiwemo nishati jadidifu na rafiki kwa mazingira.
  • Kutoa semina na warsha kwa vijana na wananchi kuhusu fursa za kiuchumi katika sekta ya nishati safi
  • Kutoa taarifa kuhusu mikopo, mafunzo, na miradi ya serikali inayolenga kukuza matumizi ya nishati endelevu.
  • Kutoa ushauri na miongozo kwa washiriki wa tamasha na wadau wa maendeleo kuhusu sera za nishati
  • Kufafanua juhudi za serikali katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), hasa SDG 7: Nishati safi na nafuu kwa wote.
  • Kushirikiana na wadau wa kimataifa na sekta binafsi kuendeleza ajenda ya nishati endelevu barani Afrika
  • Kupitia makongamano na majadiliano ya wataalamu ndani ya tamasha, pamoja na kuwezesha uwekezaji wa pamoja.

CONTACT:

 

 

Maudhui na Burudani

 

  • Uratibu wa Maudhui ya Tamasha, Kuweka mpango wa jumla wa maudhui yote yatakayowasilishwa katika tamasha (simulizi, mihadhara, mijadala, video, maonyesho, n.k).
  • Kusimamia uteuzi wa mada; waandishi wa maudhui, watangazaji na watoa mihadhara. Kuhakikisha kuwa maudhui yanalingana na malengo ya kihistoria, kielimu na kiutamaduni ya JUKANYE.
  • Burdani na Sanaa za Jukwaani; Kuandaa ratiba ya burudani ikijumuisha muziki wa asili, wa kisasa, ngoma za jadi, maigizo, mashairi na sanaa nyingine.
  • Kuratibu ushiriki wa wasanii wa ndani na wa kimataifa wanaohusiana na maudhui ya ukombozi, uzalendo, amani na mshikamano wa Afrika.
  • Kuweka viwango vya ubora na ujumbe wa kisanaa unaotolewa na wasanii.
  • Usimamizi wa Watumbuizaji na WasaniiKuwasiliana na vikundi vya burudani, wasanii binafsi, wanamuziki, na vikundi vya maigizo kuhusu mahitaji yao ya kiufundi na kisanii.
  • Kuhakikisha mahitaji ya wasanii yamezingatiwa (stage setup, sound, rehearsals, time slots, hospitality).
  • Kusimamia maadili na nidhamu ya burudani ili kuendana na heshima ya tukio.
  • Uundaji wa Ratiba ya Tamasha (Program Line-up); Kutengeneza ratiba yenye mtiririko mzuri wa matukio kwa kila siku ya tamasha.

  • Kushirikiana na timu ya itifaki, walimu wa historia, na waandaaji wa semina na makongamano.
  • Maudhui ya Kidijitali na Rekodi za Tamasha' Kuratibu uundaji wa maudhui ya video, nyaraka, podcast au vipindi vya TV kuhusu tukio na viongozi wa kihistoria.
  • Kuhakikisha maudhui yote yanahifadhiwa kwa matumizi ya baadaye na marejeo ya kihistoria.
  • Ubunifu wa Tukio na Uzoefu wa Washiriki
  • Kuweka mpangilio wa matukio ya kuvutia na yenye kusisimua kwa hadhira.

  • Kuhakikisha wageni wa tamasha wanapata uzoefu wa kipekee, wa kielimu na burudani.

CONTACT:

 

 

Brand and Marketing 

  • 1. Usimamizi wa Chapa ya Tamasha (Brand Management):
  • Kuunda na kusimamia utambulisho rasmi wa tamasha (brand identity), ikiwemo nembo, rangi, kaulimbiu na mwonekano wa kisasa wa JUKANYE.
  • Kuhakikisha kuwa chapa ya tamasha inaendana na maadili, historia na malengo ya tamasha.
  • Kusimamia ulinganifu wa chapa kwenye vifaa vyote vya mawasiliano, maonyesho, matangazo na mitandaoni.
  • 2. Mkakati wa Masoko (Marketing Strategy):
  • Kubuni na kutekeleza mikakati madhubuti ya masoko ili kuongeza uelewa na ushiriki wa watu katika tamasha.
  • Kulenga hadhira ya ndani ya nchi, bara la Afrika na kimataifa kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano.
  • Kufanya tafiti za soko ili kuelewa mahitaji ya wadau na kujua namna bora ya kuwafikia.
  • 3. Matangazo na Uhamasishaji (Advertising & Promotion):
  • Kupanga kampeni za matangazo kwenye TV, redio, magazeti, majukwaa ya kidigitali, mitandao ya kijamii na mabango ya mitaani.
  • Kushirikiana na waandishi wa habari, watangazaji, influencers na media houses kwa ajili ya kuhamasisha tamasha.
  • 4. Ushirikiano na Wadhamini (Sponsorship & Partnerships):
  • Kuandaa nyaraka za kibiashara na pendekezo la wadhamini (sponsorship proposal).
  • Kusaka wadhamini na kushirikiana nao kwa kutumia nafasi ya tamasha kukuza chapa zao.
  • Kuhakikisha kuwa wadhamini wanaonekana na kuthaminiwa ipasavyo kwenye matangazo na matukio ya tamasha.
  • 5. Usimamizi wa Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii (Media & Social Media Management):
  • Kusimamia kalenda ya maudhui (content calendar) kwa mitandao ya kijamii na kuhakikisha mawasiliano yanaendana na ujumbe wa tamasha.
  • Kuandaa taarifa kwa vyombo vya habari, matangazo ya video, mabango, vipeperushi na nyenzo za kidigitali.
  • Kufuatilia usikivu na ushawishi wa kampeni kupitia ripoti na takwimu.
  • 6. Utafiti na Tathmini (Monitoring & Evaluation):
  • Kupima mafanikio ya kampeni za masoko na kuboresha pale inapobidi.
  • Kukusanya mrejesho kutoka kwa washiriki na wadau kuhusu taswira ya tamasha na kiwango cha uhamasishaji.

MAWASILIANO:

S.L.P 38012

Dar Es Salaam, Tanzania

Mob. +255 (0) 673 023 547

Mob. +255 (0) 789 388 232

Wajumbe wa Bodi:

 Kamati kuu ya tamasha itajumuisha wajumbe kutoka JACI, Catz Company Limited, viongozi wa sekta mbalimbali za serikali, mashirika ya kimataifa, na wataalamu kutoka sekta ya Utamaduni, Nishati, Utalii na Elimu. 

Majukumu

 

  • Kuratibu Mialiko Rasmi:
  • Kuandaa na kutuma mialiko kwa wageni wa heshima wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa, mabalozi, mashujaa wa ukombozi, wasanii, na wadau wakuu wa tamasha.
  • Kuhakikisha Itifaki Inazingatiwa:
  • Kuratibu mapokezi ya wageni maalum kwa kufuata taratibu za heshima na hadhi zao.
  • Kuhakikisha taratibu za kitaifa na kimataifa za itifaki zinafuatwa ipasavyo kwenye hafla rasmi.
  • Kurahisisha Uratibu wa Wageni Maalum:
  • Kupanga ratiba, usafiri, malazi, na ulinzi wa wageni mashuhuri wanaoshiriki tamasha.
  • Kuwapa taarifa muhimu wageni kuhusu programu ya tamasha na mahitaji yao binafsi.
  • Kuhakikisha Uwasilishaji Bora wa Hotuba na Heshima:
  • Kusimamia mpangilio wa hotuba, utoaji wa tuzo, na matukio mengine ya hadhi ya juu.
  • Kuandaa watangazaji au wahudumu wa hafla wenye uelewa wa lugha na mila za itifaki.
  • Kuwezesha Ushirikiano wa Kimataifa:
  • Kufanikisha ujio na ushiriki wa wageni kutoka nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kusaidia utoaji wa viza na taarifa za kiusalama na mahitaji maalum.

Majukumu

 

  • Kuratibu Mialiko Rasmi:
  • Kuandaa na kutuma mialiko kwa wageni wa heshima wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa, mabalozi, mashujaa wa ukombozi, wasanii, na wadau wakuu wa tamasha.
  • Kuhakikisha Itifaki Inazingatiwa:
  • Kuratibu mapokezi ya wageni maalum kwa kufuata taratibu za heshima na hadhi zao.
  • Kuhakikisha taratibu za kitaifa na kimataifa za itifaki zinafuatwa ipasavyo kwenye hafla rasmi.
  • Kurahisisha Uratibu wa Wageni Maalum:
  • Kupanga ratiba, usafiri, malazi, na ulinzi wa wageni mashuhuri wanaoshiriki tamasha.
  • Kuwapa taarifa muhimu wageni kuhusu programu ya tamasha na mahitaji yao binafsi.
  • Kuhakikisha Uwasilishaji Bora wa Hotuba na Heshima:
  • Kusimamia mpangilio wa hotuba, utoaji wa tuzo, na matukio mengine ya hadhi ya juu.
  • Kuandaa watangazaji au wahudumu wa hafla wenye uelewa wa lugha na mila za itifaki.
  • Kuwezesha Ushirikiano wa Kimataifa:
  • Kufanikisha ujio na ushiriki wa wageni kutoka nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kusaidia utoaji wa viza na taarifa za kiusalama na mahitaji maalum.