Nani Anaweza Kushiriki?
Matukio na Shughuli Kuu za Tamasha la JUKANYE 2026
Maonesho ya Makumbusho ya Historia ya Viongozi wa Afrika
Yatahusu maisha, fikra na mchango wa viongozi mashuhuri kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Nelson Mandela, Kwame Nkrumah na wengine waliopigania uhuru wa Afrika.
Burdani za Muziki wa Asili na Kisasa kutoka Mataifa Mbalimbali
Vikundi mbalimbali vya muziki kutoka ndani na nje ya Afrika vitatumbuiza kwa nyimbo za asili na kisasa zenye ujumbe wa umoja, uzalendo na maendeleo.
Michezo ya Kuigiza Maudhui ya Historia
Tamthilia zenye kuelezea harakati za ukombozi wa Afrika na changamoto zilizokuwepo, zitakazosaidia kuibua uelewa wa kihistoria kwa njia ya sanaa.
Maonyesho ya Mavazi ya Kitamaduni na Tamaduni za Nchi Shiriki
Kila nchi shiriki itaonesha utajiri wa mavazi na mila zao, kudhihirisha utofauti na mshikamano wa bara la Afrika.
Makongamano kwa Vijana na Wadau wa Historia
Majadiliano ya kitaalamu yatatoa fursa kwa vijana na wataalamu kuchambua masuala ya maendeleo, ukombozi wa kisiasa na kiuchumi barani Afrika.
Kliniki ya Afya kwa Jamii
Huduma za afya bure kwa jamii zitapatikana, ikiwa ni sehemu ya kukuza maendeleo ya watu kupitia huduma bora za afya.
Ziara za Historia: Butiama, Tabora, Dar es Salaam na Mikoa ya Kusini
Ziara maalum kwenye maeneo yenye historia ya harakati za ukombozi kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.
Ziara za Kitalii
Utembeleaji wa vivutio vya utalii kama Mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar, hifadhi za Taifa, mapori ya akiba, misitu na makumbusho.
Kampeni ya Matumizi ya Nishati Salama ya Kupikia
Elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutumia nishati salama na rafiki kwa mazingira majumbani na katika biashara.
Uzinduzi wa Makala Maalum ya Mwalimu Julius Nyerere
Filamu au makala mahsusi kuhusu maisha, falsafa na mchango wa Baba wa Taifa kwa maendeleo ya Afrika.
Madarasa ya “Tuseme Kiswahili” kwa Wageni kutoka Mataifa Mbalimbali
Fursa kwa wageni kujifunza Kiswahili, ili kuongeza matumizi ya lugha hii kama chombo cha mawasiliano barani Afrika.
Utoaji wa Tuzo za Heshima
Kuwatambua na kuwapa heshima viongozi wa zamani na wa sasa, wanamuziki, na watu waliotoa mchango mkubwa katika kuhamasisha uzalendo, amani, na maendeleo kupitia kazi zao.
🔥 Miliki Ushujaa. Dhamini Tamasha.
Kwa kuvaa bidhaa za JUKANYE, Utakuwa:
Unaunga mkono Tamasha la Kimataifa la Historia la JUKANYE na dhamira yake yenye nguvu ya kuhamasisha, kuelimisha, na kuunganisha.
Unasaidia kufadhili programu za uwezeshaji wa vijana, uhifadhi wa urithi wa utamaduni, umoja wa Afrika, na elimu ya historia.
Kila T-shirt, Kofia, na Kitenge unachonunua si vazi pekee — ni tamko la uzalendo, heshima kwa mashujaa wetu, na mchango kwa mustakabali wa urithi wa Afrika.
Vaa Mitindo inayohamasisha Uhuru.
Vaa Roho ya Uzalendo. Eneza Nguvu za Tamasha."
Vaa Roho ya Uzalendo. Eneza Nguvu za Tamasha."
You will find the latest information about us on this page. Our company is constantly evolving and growing. We provide wide range of services. Our mission is to provide best solution that helps everyone. If you want to contact us, please fill the contact form on our website. We wish you a good day!
Jivike Urithi. Sherehekea Tamasha.